Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager, wamewataka watanzania kutokata tamaa licha ya Taifa Stars kutofuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani kwani timu imeonesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa. Ombi hilo lilitolewa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe wakati alipowaandalia Taifa Stars chakula cha jioni katika hoteli ya Tansoma ikiwa ni utaratibu wa wadhamini hao kama njia ya kuwakaribisha wachezaji kambini. Alisema bado kuna mashindano mengine kama CHAN na AFCON ambayo wana imani Taifa Stars itafuzu na kwuweka historia. Aliwaasa wachezaji kuhakikisha wanashinda mechi dhidi ya Uganda haa nyumbani na pia watakapoenda Uganda baadaye mwezi huu katika mechi ya kuwania kufuzu mashindano ya CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.

Comments

Popular Posts