BINTI NUSURU ACHANIWE NGUO KWA KUVAA NGUO ZISIZO ...
BINTI NUSURU ACHANIWE NGUO KWA KUVAA NGUO ZISIZO NA MAADILI YA KITANZANIA
Hapa binti huyo akijificha kupigwa picha eneo la Tanesco |
Hapa akikimbia kuelekea stendi ya daladala miyombini mjini Iringa |
Hapa akijificha kwa kijana huyu ili kukwepa picha |
Hapa akiamua kuondoa eneo hilo |
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10.45 jioni baada ya binti huyo kushuka katika daladala ya Mkwawa kwenye stendi hiyo ya M.R iliyopo kata ya Miyomboni na baada ya mmoja kati ya wananchi kumwita na kumuonya juu ya nguo hizo binti huyo alianza kutoa lugha chafu kuwa ana uhuru wa kuvaa hivyo ndipo songombingo lilipotokea kwa vijana kutaka kumwadabisha kwa kumfukuza ili kumchania nguo hiyo .
Hata hivyo binti huyo anayekadiliwa umri wa miaka 18 ama 20 alilazimika kutimua mbio na kwenda kujificha katika moja kati ya vibanda vinavyouza viatu katika eneo la Tanesco na kujificha hapa hadi wananchi hao walipoamua kumsamehe na kuendelea na shughuli zao.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya mashuhuda walisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa na sifa mbaya ya maambukizi makubwa ya VVU na kwa sehemu wanaochangia maambukizi hayo ya wanawake ambao wanatembea nusu uchi na kuchangia kuhamasisha ngono kwa vijana.
Hivyo wameiomba serikali ya mkoa wa Iringa kutunga sheria ndogo zinazozuia mavazi yasiyo na maadili kuvaliwa machana katika maeneo ya wazi kama hivyo na wale wanaotembea nusu uchi kuwajibishwa .
Comments
Post a Comment