SENENE ZALETA KIZAA ZAA IRINGA, WALIMU WADAIWA K...
December 11, 2012
SENENE ZALETA KIZAA ZAA IRINGA, WALIMU WADAIWA KUTOA ADHABU YA KUKUSANYA SENENE KWA WANAFUNZI
wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa wakienda shule na senene |
Gari lenye namba za usajili T 356 BXK likiwa limebeba senene kupeleka sokoni Iringa kuuza |
Kijana akiwa amebeba magunia ya Senene katika mkokoteni akielekea kusaka wateja |
Senene wakiwa wamezagaa katika jengo la Asas |
Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika mji wa Iringa imeshusha neema kwa wakazi wa mji wa Iringa ambao ni wapenzi wa Senene baada ya baadhi ya wamiliki wa nyumba kudaiwa kuwazuia wapangaji wao kuokota senene katika nyumba zao huku walimu pamoja na watumishi wa umma wakichelewa kuingia makazini kutokana na zoezi la kuokota senene hao.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi katika shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa asubuhi ya jana umebaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi na walimu wao walionekana katika maeneo ya shule hizo wakikusanya senene huku baadhi ya wazazi wakilalamikia baadhi ya walimu kuwapa adhabu ya kukamata senene kwa wanafunzi waliochelewa kufika shule.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi katika shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa asubuhi ya jana umebaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi na walimu wao walionekana katika maeneo ya shule hizo wakikusanya senene huku baadhi ya wazazi wakilalamikia baadhi ya walimu kuwapa adhabu ya kukamata senene kwa wanafunzi waliochelewa kufika shule.
Mmoja kati ya wazazi ambaye alijitambulisha kwa jina la Jackson Ndelwa alisema kuwa anashangazwa na utaratibu wa walimu wa shule mbali mbali za msingi katika Manispaa ya Iringa kuwaacha wanafunzi wakiendelea kukamata senene katika maeneo ya shule hadi mida ya saa 4 asubuhi wakati kwa kawaida muda huo wanafunzi wanapaswa kuwa madarasani .
Hivyo aliuomba uongozi wa elimu katika Manispaa ya Iringa kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi na walimu wao kwa siku ya jana na iwapo itabainika kuwa wanafunzi hawakuingia madarasani kwa ajili ya kufanya shughuli za kukamata senene za walimu basi walimu waliohusika kuwapa wanafunzi adhabu ya kukamata senene wakati wa mvua kuchukuliwa hatua kali.
Mmoja kati ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa ambae aliomba jina lake na shule yake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa walimu mjini Iringa alisema kuwa madai ya wazazi kuhusu wanafunzi kutumwa na walimu wao wa madarasa kuokota senene ni ya kweli na kuwa badhi ya walimu na wanafunzi kwa muda wa asubuhi walikuwa wakishindana kufukuza senene kama kitoweo .
Pia alisema kwa siku ya jana hata adhabu za kawaida ambazo walimu wamekuwa wakizitoa kwa wanafunzi wanaochelewa kama adhabu ya viboko haikuwepo na badala yake wanafunzi waliochelewa walikuwa wakipewa adhabu ya kukusanya senene kwa ajili ya kitoweo cha walimu na sehemu ya senene wanafunzi wamekuwa wakipewa .
Wakati wazazi wa wanafunzi hao wakilalamikia hatua ya walimu wa shule za msingi kuwatumia wanafunzi katika kuokota senene kwa upande wao baadhi ya wamiliki wa nyumba katika mji wa Iringa wamedaiwa kuwanyanyasa wapangaji wao kwa kuwazuia kuokota senene zinazoanguka katika nyumba zao kwa madai kuwa senene hizo ni mali ya mwenye nyumba na iwapo wanataka basi kutoka nje ya uzio wa nyumba hizo usiku kwenda kusaka senene mitaani .
Mbali ya wanafunzi hao na baadhi ya wamiliki wa nyumba mjini Iringa kuonyesha kugombea senene hao badhi ya wananchi wameweza kunufaika zaidi ya senene hao kwa kuokota magunia kwa magunia ya senene na kuwauza kati ya shilingi 35,000 hadi 50,000 huku walinzi wa maeneo mbali mbali ya biashara mjini hapa wakiacha malindo yao na kukusanyika eneo la jengo la mfanyabiashara Salim Abri Asas kukusanya senene hadi mida ya saa 7 mchana kutokana na eneo hilo kuwekwa taa zenye mwanga mkali zaidi.
Comments
Post a Comment