MKURUGENZI

MKURUGENZIwa Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Obeid Mbangwaamesimamishwa kazi kuanzia jana kupisha uchunguzi kuhusu wanyamapori 120 nandege 16 waliotoroshwa Novemba mwaka jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifawa Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige amelieleza Bunge kuwa, Mbangwaamesimamishwa kazi na watumishi wengine wawili wa Wizara hiyo lakini hakuwatajaili kutoathiri uchunguzi. Maige amewaeleza wabunge kuwa, Mbangwa ataendelea kulipwa, na wote waliohusikakutorosha wanyama na ndege hao watafikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa Maige, Wizara hiyo inashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalamakuchunguza utoroshaji huo, na kwamba, watu sita tayari wameshitakiwa katikaMahakama mjini Moshi kwa tuhuma za kuhujumu uchumi. Waziri Maige amewaeleza wabunge kuwa, ndege ya jeshi la Qatar iliyowatoroshawanyama na ndege hao ilikuja nchini kihalali kwa kuwa ilikuwa na kibali chakumleta mwanadiplomasia nchini kwa safari binafsi. Amesema, ndege hiyo ilionekana kwenye vyombo vya usalama, lakini haikukaguliwawakati inaondoka na hadi sasa haijulikani wanyama na ndege hao walipelekwawapi. Maige amewaeleza wabunge kuwa, biashara ya kukamata wanyama na kuwasafirishanje ya nchi ni halali, kampuni 180 zina leseni, na kwamba, waliokamatamaliasili zilizotoroshwa walikuwa na vibali vyote muhimu vilivyowaruhusukukamata na kumiliki wanyama hao lakini ukaguzi ulipofanywa hawakuonekana. Amesema, Wizara inashirikiana na vyombo vya ulinzi na upelelezi vya kimataifalikiwemo shirika la Interpol ili kufahamu nyaraka zilizotumika kuwasafirishawanyamapori na ndege, walipelekwa wapi na wapo kwa nani hivi sasa. Ameomba wabunge wenye taarifa kuhusu utoroshaji huo wampe taarifa na anaaminiwanamuamini, wakishindwa wawape mawaziri wengine, na endapo taarifa hizohazitatumika ipasavyo wamuwajibishe bungeni. Maige amesema bungeni kuwa, kutoroshwa kwa ndege na wanyama hao kumemkasirishakuliko jambo lingine lolote katika utumishi wake wa umma. Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira jana ilihojiilichodai kuwa ni kigugumizi cha Serikali kuhakikisha kuwa wanyamapori 116 haina ndege 16 walioibwa nchini Novemba 24 mwaka jana wanarudishwa nchini. Kamati hiyo ililieleza Bunge kuwa, wanyama hao wakiwemo twiga wanne na ndegehai ambao wana jumla ya thamani ya Sh. 170,570,500 waliibwa kwa kutumia ndegeya jeshi la Qatar kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Bunge lilielezwa kuwa, wanyamapori walioibwa wana thamani ya Sh.163,732,500.00/- na ndege hai wana thamani ya Sh. 6,838,000.00/- Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli alisema, hadi jana kamati ilikuwahaifahamu wanyama na ndege hao walipelekwa wapi na kama bado wapo hai. Aliyasema hayo wakati anasoma taarifa ya kamati kuhusu utekelezaji wa majukumuya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2010/2011 pamoja na maoni ya kamatikuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2011/2012. Lembeli alisema, uharamia huo ulifanywa na Watanzania na kwamba, kigugumizi chaSerikali kushughulikia suala hilo kimeisikitisha Kamati kwa kuwa rasilimaliiliyoibwa ni adimu na haijulikani itarudishwa lini nchini. “Kwa hakika kuna dalili kubwa ya uzembe na kulindana ndani ya Wizara hii nandiyo maana kumekuwa na kigugumizi katika kushughulikia ushauri wa kamati.Ukweli wa mashaka haya unajidhihirisha katika zoezi zima lililofanyika hivikaribuni ndani ya idara husika la kuhamisha maafisa” alisema Lembeli. Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige amelieleza Bunge kuwa, wanyama haiwa aina mbalimbali 120 na ndege hai 16 walitoroshwa Novemba 26 mwaka 2010kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Comments