Umoja wa Mataifa unasema mashirika ya misaada yanahitaji dola milioni 166 kuwasaidia raia nchini Sudan ya Kusini huku taifa hilo jipya barani Afrika likihofiwa kuingia kwenye vita vya kikabila.


Fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu, chakula, na pia kuongoza kambi za wakimbizi wa ndani, kwa mujibu wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kiutu ya Umoja wa Mataifa. Vile vile zitatumika kwa ajili ya wakimbizi 200,000 wa Sudan ambao wamekimbia kwenye majimbo ya Unity na Upper Nile ya Sudan ya Kusini. "Kuna kiasi cha wakimbizi wa ndani 90,000 waliotokana na mapigano ya siku kumi zilizopita. Hao ni pamoja na 58,000 waliojihifadhi kwenye majengo ya Umoja wa Mataifa," alisema Toby Lanzer, mratibu wa huduma za kiutu za Umoja wa Mataifa nchini Sudan ya Kusini. "Hiki ni kipindi kigumu sana kwa watu wa taifa hili jipya, na ni muhimu sana kwa mashirika ya misaada kuwa na fedha yanayohitaji kuokoa maisha ya watu," aliongeza, akielezea matarajio yake kuwa wafadhili watachukua hatua za haraka kupata fedha hizo.

Comments

  1. http://www.youtube.com/watch?v=xv8DBmLnqVM

    http://www.youtube.com/watch?v=re9lEsg24Fk

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts