DEREVA WA BASI LA MSANYA TRANS LILILOUA 11 IRINGA...

DEREVA WA BASI LA MSANYA TRANS LILILOUA 11 IRINGA ASOMEWA MASHTAKA 40 AKIWA WODINI ,AKANA YOTE


Mtuhumiwa wa ajali ya basi la Msanya Trans lenye namba  za usajili T 803 AJV Nisani Bw Rashid Selemani Msanya (35) lililosababisha vifo vya  abiria 1 na kujeruhi wengine 28 akiwa wodini katika Hospitali ya mkoa  wa Iringa baada ya  kusomewa mashtaka yake 40 na mahakama akiwa kitandani

 Wagonjwa na  ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika  wodi hilo wakishuhudia tukio  hilo baada ya hakimu  mkazi ,mwandamizi  mfawidhi  wa mahakama ya mkoa wa Iringa Juma Hasan kumaliza kushughuli za kimahakama  Hospitalini hapo 
DEREVA  wa basi la Msanya Trans  ambalo lilitapa ajali mbaya  jumamosi ya wiki  iliyopita na kusababisha  vifo vya  watu 11 na  kujeruhi wengine zaidi ya 20  katika  eneo la Kichakani kwenye barabara  kuu ya Iringa -Mbeya amesomewa mashitaka 40 akiwa wodi
ni katika Hospitali ya  mkoa  wa Iringa.
Wakisoma mashtaka  hayo  leo  katika wodi namba  5 Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa ,mbele ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi  wa mkoa wa Iringa Juma Hassan wakili wa  serikali  Adolph Maganda akisaidiwa na msaidizi  wake Hamad Magenda  alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo katika  kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2012 ya usalama barabarani anatuhumiwa kutenda makosa hayo Desemba 8 mwaka  huu .
Alisema  kuwa mtuhumiwa  huyo Bw Rashid Selemani Msanya (35) ambae alikuwa ni dereva wa basi hilo la Msanya Trans  lenye namba za usajili T 803 AJV Nissan ambalo  lilikuwa likitokea Iringa mjini kwenda Usokami  wilaya ya Mufindi alisababisha ajali  na  kupelekea vifo  vya  watu 11 waliokufa katika ajali  hiyo.
Wakili Magande alisema kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa makosa 40  ambapo jumla ya makosa 11 ni ya kusababisha  vifo na makosa 28 ni ya  kusababisha majeruhi na kosa moja kati ya 40 ni kusababisha ajali na kuharibu gari  hilo.
Hata  hivyo  mtuhumiwa  huyo amekana makosa  yote na kuendelea kuwa  chini ya ulinzi  wa  polisi wakati akiendelea  kupatiwa matibabu katika  Hospitali  hiyo ya mkoa  wa Iringa akitibiwa majeraha makubwa ya moto ambao unasadikika  kutokana na maji ya rejeta ya basi hilo.
Hakimu  wa mahakama hiyo mheshimiwa Hassan alimnyima  dhamana mtuhumiwa  huyo hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Desemba 20 mwaka  huu na kuwa mtuhumiwa ataendelea  kuwa chini ya ulinzi  wa polisi katika Hospitali  hiyo.
DEREVA WA BASI LA MSANYA TRANS LILILOUA 11 IRINGA...: Mtuhumiwa wa ajali ya basi la Msanya Trans lenye namba  za usajili T 803 AJV Nisani Bw Rashid Selemani Msanya (35) lililosababisha vi...

Comments