Watu wengi wamekuwa wakijali zaidi uso.
Shingo ni kiungo kilichokuwa hakitiliwi mkazo katika suala zima la urembo. Watu wengi wamekuwa wakijali zaidi uso, kucha, ngozi na maeneo mengine wanahisi ni muhimu kwao.
Lakini, ukweli ni kwamba, shingo ni kiungo muhimu na kinapaswa kuangaliwa kwa umakini kama ilivyo uso kwa kuwa ni miongoni mwa viungo ambavyo huonekana kwa haraka zaidi.
Kutokana na hilo, unapaswa kuhakikisha mwonekano wako wa juu unaenda sanjari na shingo, ili kuepusha tofauti ya aina yoyote itakayosababisha kupunguza au kuondoa kabisa mvuto wako.
Haitaleta maana ikiwa utapendeza kichwani na usoni, lakini shingo yako ikawa na mikunjo au uchafu unaoweza kuondololewa, tena kwa njia za asili. Ngozi ya shingo ni lainizaidi, hivyo epuka kuipaka vipodozi vyenye kemikali kwani huenda vikaiharibu na kupoteza mvuto wake wa asili.
Comments
Post a Comment