Kenya, Uganda na Rwanda
Serikali imeziomba nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuipa taarifa ya mikutano waliyoifanya bila ya kuishirikisha hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumzia na waandishi wa habari ofisini kwake alisema wameziomba nchi hizo kuitaarifu kile walichokijadili.
Alisema kwakuwa nchi hizo ni miongoni mwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zilitakiwa kutoa maelezo kwa Umoja huo ili kila nchi wanachama ziweze kutambua lengo lao.
Comments
Post a Comment