Maafisa wa Umoja wa Ulaya wameitaka Uturuki kushughulikia kashfa ya rushwa.


Maafisa wa Umoja wa Ulaya wameitaka Uturuki kushughulikia kashfa ya rushwa inayozidi kukuwa kwa njia ya uwazi kutokana na kuwepo kwa wasi wasi kwamba serikali inajaribu kuzima uchunguzi ambao umewalenga watu walio karibu na Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan. Erdogan wiki hii alilibadilisha baraza la mawaziri na kuwatimuwa mawaziri muhimu baada ya watu 24 wakiwemo watoto wa kiume wa mawaziri wawili wa zamani kukamatwa kwa madai ya rushwa. Lakini kiongozi huyo wa Uturuki pia amedai kwamba serikali yake ni muhanga wa njama ya kigeni na ya ndani ya nchi kuiyumbisha Uturuki na amechukuwa hatua ambazo wapinzani wanasema zinakusudia kukwamisha uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa maafisa wa polisi kwenye nyadhifa zao. Erdogan pia amebadili taratibu za polisi kuhakikisha kwamba uchunguzi wa masuala ya rushwa unapitia kwa viongozi wa juu wa polisi na mahakama walio karibu na serikali lakini mahakama kuu ya Uturuki imeutanguwa uamuzi huo.

Comments