BINTI NUSURU ACHANIWE NGUO KWA KUVAA NGUO ZISIZO ...

BINTI NUSURU ACHANIWE NGUO KWA KUVAA NGUO ZISIZO NA MAADILI YA KITANZANIA


Hapa binti  huyo akijificha  kupigwa  picha  eneo la Tanesco
Hapa akikimbia  kuelekea  stendi ya  daladala  miyombini mjini Iringa
Hapa akijificha kwa  kijana  huyu ili kukwepa picha
Hapa akiamua  kuondoa eneo hilo
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida binti mmoja ambaye jina limehifadhiwa na mtandao huu amejikuta katika wakati mgumu hii leo katika eneo la stendi ya M.R mjini Iringa baada ya kuvaa nguo zisizo na maadili ya kitanzinia zenye  kuonyesha nyeti  zake .

Tukio  hilo  limetokea  majira ya saa 10.45 jioni  baada ya  binti huyo kushuka katika daladala ya Mkwawa kwenye stendi hiyo ya M.R iliyopo kata ya Miyomboni na baada ya  mmoja kati ya  wananchi kumwita na kumuonya juu ya nguo hizo binti  huyo alianza kutoa  lugha chafu  kuwa ana uhuru  wa kuvaa hivyo ndipo  songombingo  lilipotokea kwa  vijana  kutaka  kumwadabisha kwa kumfukuza  ili kumchania  nguo  hiyo .

Hata hivyo  binti  huyo anayekadiliwa umri  wa miaka  18 ama 20 alilazimika  kutimua mbio na kwenda  kujificha katika  moja kati ya vibanda  vinavyouza  viatu katika eneo  la Tanesco na kujificha hapa hadi wananchi hao  walipoamua  kumsamehe na kuendelea na shughuli zao.

Wakizungumza na mtandao  huu  baadhi ya mashuhuda  walisema  kuwa mkoa  wa Iringa  umekuwa na sifa mbaya ya  maambukizi  makubwa ya VVU na  kwa sehemu  wanaochangia maambukizi hayo ya  wanawake ambao  wanatembea nusu uchi na  kuchangia kuhamasisha ngono kwa  vijana.

Hivyo  wameiomba  serikali  ya  mkoa  wa Iringa kutunga  sheria ndogo  zinazozuia mavazi yasiyo na maadili  kuvaliwa machana katika maeneo ya  wazi kama hivyo na  wale  wanaotembea nusu uchi kuwajibishwa .


Comments